Mayness's Blogu za marafiki

Yaliyojiri Mlimani City Shopping Carnival

//added by kai userpoints:upperplural

November 28, 2009 na Kai   Maoni (0)

Maonesho ya bidhaa yaliyo ambatana na punguzo la bei yaliyopewa jina la Mlimani City Shopping Carnical yamemalizika jana usiku. Yalikuwa ni maonesho ya aina yake ambayo yametumika kama sherehe za kuadhimisha miaka mitatu tangu kufunguliwa kwa Mlimani City. Pamoja na kupata punguzo la bei katika maduka kadhaa pale ndani ya jengo la mlimani city pia watu wengi walivutwa na burudani iliyokuwa inatolewa nje ya jengo, sehemu ya kupaki magari.

Nikianzia na burudani, maonesho yamewapatia fursa baadhi ya vijana kuonesha vipaji vyao. Kulikuwa na mashindano ya kuimba muziki wa kizazi kipya, uwezo ulio oneshwa na washiriki unathibitisha kwamba bado kuja vijana wengi wenye uwezo mtaani. Nadhani kama ningekuwa ninahusika na uandaaji wa muziki ningepata walau hata mmoja wa kuingiza kwenye lebo yangu. Kwa kuwa sihusiki na muziki nilibaki kufurahia tu. Makundi ya uchezaji wa muziki yalileta uhai katika maonesho hayo, uwezo na ubunifu ulio oneshwa unathibitisha kwamba ni wakati muafaka wa kuibua tena moto wa sanaa ya uchezaji kama ilivyokuwa miaka ile...

Nilihudhuria tamasha hilo la kutimiza miaka mitatu kwa siku tano mfululizo, na zaidi nilivutwa na banda la KENICE POOL TABLE, kwa kuwa mimi pia ni mchezaji wa mchezo wa pool table nilikuwa pale  kuangalia na kucheza mchezo huo na watu kutoka sehemu mbali mbali ili kujipima ubavu. Nilipata bahati ya kushiriki mashindano mawili tofauti hata hivyo sikuweza kufurukuta mbele ya viwango vilivyokuwa pale. Hata hivyo nilipenda ubora wa meza zao.

Makampuni yanayotoa huduma za siku (TIGO na VODACOM) yalikuwepo kusajiri laini za wateja wao, dhana hii ya kusogeza huduma ya usajiri wa laini za simu karibu zaidi na wananchi imesaidia sana kupunguza misongamano na foleni sehemu za kusajiria, sijui kama na nje ya Dar es salaam iko hivi ama ni hapa tu.

Kulikuwa  na maduka na makampuni mengi yaliyoshiriki,  na shughuli nyingi zilizokuwa zinaendelea, nimekuletea yale yaliyo onekana kuvuta watu wengi hasa pale kwenye maegesho ya magari.

Dr. Aman Abeid Karume apata Shahada ya Heshima ya Uzamivu (honoris causa).

//added by kai userpoints:upperplural

November 14, 2009 na Kai   Maoni (0)

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Aman Abeid Karume amepata shahada ya heshima ya uzamivu kutoka chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki. Mkuu wa Chuo Dk. Salim Hamed Salim amemtunuku Dr. Karume shahada hiyo ya uzamivu  leo tarehe 14/11/2009 kwenye mahafali ya saba ya chuo hicho.

Akisoma wasifu wa Mheshimiwa Dk. Karume, Prof. Msamati wa Chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki amesema Dk. Karume amepewa heshima hiyo kutokana na kutokomeza ugonjwa wa malaria visiwani Zanzibar.

Utapata habari zaidi na picha

SIMBANET imejiunga na SEACOM

//added by kai userpoints:upperplural

August 13, 2009 na Kai   Maoni (1)

Kampuni ya Simbanet imeunganishwa na mkonga wa SEACOM. Uzinduzi huo umefanywa na Makamu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dkt. Maua Daftari. SimbaNet imekuwa kampuni binafsi ya kwanza kujiunga na mkonga huo unaopita chini ya bahari na kuunganisha nchi za kusini na Mashariki mwa Afrika. Kampuni ya kwanza kujiunga na SEACOM ilikuwa TTCL iliyojiunga mwishoni mwa mwezi uliopita.

 

Nichague simu gani?

//added by kai userpoints:upperplural

July 4, 2009 na Kai   Maoni (0)

Kuna ina nyingi sana za simu, zenye majina kibao, simu nyingine hazina hata majina. Kuna ambazo zinazosemekana kuwa feki nyingine halisi. Changamoto iliyopo ni kujua ipi feki na ipi halisi. Hilo nakuachia wewe.

Kabla ya kununua simu angalia mtandao unaotumia, angalia vitu au huduma wanazotoa. Chagua simu yenye  yenye vitu (features) zinazoendana na mtandao wako, maana kwa mfano unaweza kununua simu yenye Video call lakini mtandao wako hauna hiyo huduma, hiyo ina maana utakuwa umelipa pesa zaidi ili kupata huduma ambayo hautaitumia.

Kuna simu za aina nyingi zenye muonekano na uwezo tofauti. Kama utakuwa unatumia simu yako mara kwa mara, chagua simu yenye uwezo mkubwa.

Kuwa makini unapochagua simu zinazotolewa na makampuni ya simu kwa bei nafuu, maana mara nyingi zinakuwa na vitu vichache pengine kuliko mahitaji yako.

Angalia ukubwa na uzito wa simu, fikiri wapi utakuwa unaiweka simu kwa muda mrefu, mfukoni? Kwenye mfuko wa kushikiza kwenye mkanda? Mkononi?...

Angalia uwezo ba betri ya simu unayotaka kununua, nunua simu yenye kuhifadhi chaji kwa muda mrefu. Wakati unaangalia uwezo wa betri kuna vitu viwili, “standby time” na “talk time”. Standby time ni muda simu itatumia  bila kutumika lakini ikiwa imewashwa “muda tangu imechajiwa”. Talk time ni muda ambao unaweza kutumia simu yako kuongea pindi inakuwa imechajiwa”.

 

Utajua vipi kuhusu yote haya? Ingia kwenye mtandao tafuta “phone reviews” za aina ya simu unayohitaji hapo utaelezwa kila kitu kuhusu hiyo simu na watumiaji wengine ambao wamekutangulia kununua.

 

Sitazungumzia majina ya simu maana hapo kila mmoja ana uchaguzi wake, binafsi kitu ninacho angalia ni sifa nilizotaja hapo juu na wala siyo jina la simu.

Kwa sasa ninatumia PRADA KE850, Je wewe unatumia simu gani? Unaipenda? Kama ukipewa nafasi ya kuchagua simu kwa sasa utachagua aina hiyo tena? Unadhani ulifanya kosa kununua hiyo simu. Niambie ni simu gain unaizimia hata kama haujapata bahati ya kuwa nayo.

 

Michael Jackson Afariki

//added by kai userpoints:upperplural

June 25, 2009 na Kai   Maoni (0)

Michael Joseph jackson alizaliwa 29/8/1958 amefariki 25/6/2009. Alikuwa ni Mwanamuziki, mtoto wa saba katika familia yao, alianza muziki akiwa na umri wa miaka 11 akiwa katika kundi la Jackson 5. alianza kufanya muziki peke yake mwaka 1971 wakati huo huo akiendeleea na kundi lake la Jackson 5. Akijulikana kama Mfalme wa POP alitoa alubam kadhaa zikiwemo Thriller, Bad, Dangerous na Off the wall.

Soma zaidi hapa http://en.wikipedia.org/wiki/Michael_Jackson

 

Misamiati

//added by kai userpoints:upperplural

June 19, 2009 na Kai   Maoni (0)

,

Ifuatayo ni misamiati ya kiswahilil iliyotumika katika mtandao jamii huu.

  • Alamisha - Bookmark
  • Sasisha - Update
  • Kokota - Drag
  • Kivinjari - Browser
  • Mwambaa - Bar
  • Kiunganishi - Link
  • Kibwedo - Favorite
  • Matini - Text
  • Bimba - Body
  • Zana - Tools
  • Kisanduku pokezi - Inbox
  • Zinzo - Display
  • Changia - Share
  • Ikoni - Icon
  • Hifadhidata - Database
  • Saraka - Directory
  • Wasifu - Profile
  • Hifadhi - Save
  • Lemaza - Disable
  • Mtumiaji - User
  • MYM (Maswali yaulizwayo mara kwa mara) - FAQ (Frequently Asked Questions)
  • Futike - embedded
  • Mkopezi - Recipient
  • Maarufu - Popular
  • Mahsusi - Specific
  • Hivi karibuni - Recent
  • Maoni - Comment
  • Jumla - General
  • Kitengo - Category
  • Utungo - String
  • Programu jalizi - Plugin
  • Badilisha - Replace
  • Uga - Field
  • Orodha - List
  • Paneli - Panel
  • Sanidi - Configure
  • Sanikisha - Install
  • Mtunzi - Author
  • Kisara (Kionyeshi Sanifu Rasilimali) - URL
  • Hadhari - Warning
  • Tangamana - Compatible
  • Vipimo - Settings
  • Ukumbi - Forum
  • Chuja - Filter