guid: 1870
type: object
subtype: 14
owner_guid: 2
container_guid: 2
time_created: 1258918809
title: Google contest
description:
Google imedhamini shindano la kuandika na kutafsiri makala za Wikipedia. Shindalo hilo linahusisha waongea kiswahili popote pale walipo. Kuna zawadi zitatolewa kwa ajili ya washindi. Tumekuwa tunasoma habari na makala mbali mbali kutoka kwenye wavuti, sasa huu ni muda wetu kuchangia.
Katika shindano hili unaruhusiwa kuandika kuhusu mada yoyote ambayo unapenda. Kama unataka kuandika mada mpya hakikisha haipo kwenye wikipedia, utajua kwamba haipo kwa kutumia kitufe cha kutafuta kwenye wikipedia, la sivyo ni rahisi kutafsiri makala. Hakuna maksi za ziada kama utaandika makala mpya. Kuna zana ya google (google toolkit) inayowezesha kutafsiri kwa urahisi zaidi.
Ili kupata habari zaidi za shindano hili bofya hapa http://www.google.com/events/kiswahili-wiki/ Mwisho wa kujisajili ni tarehe 25/11/2009.
Jisajili kwenye tovuti niliyotoa hapo juu ili upate habari zaidi, pia kuna kundi la watumiaji walio jisajili na tayari wamepata mafunzo ya kufanya kazi hiyo, hivyo kuna msaada kama utakwama mahali.
write_access_id: 2
parent_guid: 0
|
|
|
|
|


